Image thumbnail

Blog

HomeMixed GrillThe Food Challenge Documentaries (Swahili)

The Food Challenge Documentaries (Swahili)

Wasiwasi nyingi zimechipuka  kuhusu usalama wa chakula katika Kenya. Haswa, ongezeko la kewepo kwa kemikali hatari za dawa ya kuua wadudu. Angalau 33% ya dawa za kuua wadudu ambazo kwa sasa zimesajiliwa na zinauzwa katika bidhaa Kenya, zimeondolewa katika soko la ulaya kwa sababu ya madhara makubwa yanayoweza kutokea kwa afya ya binaadamu na mazingira. Zipo bidhaa katika soko la Kenya ambazo bila shaka zimeainishwa kuwa zenye uwezo wa kusababisha saratani (bidhaa 45), mabadiliko ya kimaumbile (bidhaa 31), kuvuruga mfumo wa homoni (bidhaa 51), kuathiri mfumo wa neva (bidhaa 175) na nyingi zinazoonyesha athari za wazi kwa mfumo wa uzazi (bidhaa 360). Madhara yake kwa wakulima ni makubwa na yanahofisha.

Ujuzi Media kwa msaada wa Bread for the world, Misereor, NordMedia Film Fund na Route to Food Initiative, imetoa filamu katika sehemu tatu inayoitwa “The Food Challenge”. Filamu inaonyesha waziwazi njia ambazo wakulima wadogo wadogo wanatumia na kuamini ahidi za mazao mazuri zaidi zilizotolewa na watengenezaji wa dawa hizi za wadudu. Filamu hii kwa umuhimu mkubwa inatilia shaka iwapo kemikali za kilimo zinahitajiika kwa vita dhidi ya njaa na wakati uo huo ikitoa maoni ya njia mbadala kutumiwa kwa uzalishaji wa chakula kama vile ukulima wa kiasili.

Tunawaalika kutazama filamu hizi na kuwashirikisha wengine kutazama kwa wingi kadri unavyoweza ili tuweze kuwaelimisha watu kuhusu shida hii wakati uo huo tukiwaeleza na kuendeleza njia bora za kujichagulia wanachohitaji na njia za ukulima za kudumu – kilimo cha kiekolojia, mifumo ya kilimo endelevu, kilimo asili.

Jiunge nasi kwenye mitandao kutumia #ToxicBusiness tunapoishurutisha serekali kuondoa mara moja dawa za wadudu zilizo na viungo vyenye sumu kwa afya ya binadamu na mazingira, na inahatarisha kuwepo kwa chakula na usalama wa chakula nchini.

Sehemu ya 1: Biashara ya sumu

Sehemu ya 2: Kinachosababisha njaa

Sehemu ya 3: Kutafuta uendelezaji

Post a Comment