The Route to Food Alliance - Route to Food
Food, Kenya, NGO
865
page-template,page-template-full_width,page-template-full_width-php,page,page-id-865,cookies-not-set,ajax_fade,page_not_loaded,,select-child-theme-ver-1.0.0,select-theme-ver-4.4.1,wpb-js-composer js-comp-ver-5.4.7,vc_responsive

The Route to Food Alliance

Kiswahili
  1. Ninatambua kuwa usalama wa chakula ni haki ya kibinaadamu inayopatikana katika kipengele cha 43 cha katiba ya Kenya, ambapo kila mtu, mwanamume mwanamke na mtoto ana haki ya kuwa huru kutokana na njaa na kuwa na lishe bora.
  2. Ninaelewa kwamba kuwa usalama kwa chakula haupimwi kwa kiwango cha magunia ya mahindi yaliyoko kwenye maghala ya serikali na kusema tuko salama kwa chakula bali inamaanisha zaidi ya kutokuwa na njaa.
  3. Ninakubali kwamba haki ya kibinaadamu kwa chakula si haki ya kulishwa .Ni haki ya kujilisha kwa heshima.
  4. Ninapinga kwa nguvu viongozi na walio katika ofisi za umma wanaotumia chakula au msaada wa chakula kisiasa.
  5. Ninaunga mkono mabadiliko ya sheria ya kijinsia ambayo inaimarisha nafasi ya wanawake kuwa sawa na wanaume – katika sekta za kilimo, ufugaji wa wanyama na uvuvi wa samaki.
  6. Naunga mkono viongozi wanaozingatia sera za usalama wa chakula na haki za kijamii kwa kuwekeza katika njia ndogo ndogo za kilimo, ugawaji na uzalishaji zaidi na pia kujumuisha utendakazi wa wanaume na wanawake, wazee na vijana, ambao huteseka kutokana na ukosefu wa chakula mara kwa mara.
  7. Naelewa kuwa njaa na lishe duni ni shida ya mara kwa mara na si janga la mara moja tu linalosababishwa na mabadiliko ya hali ya anga. Kwa hivyo ninaunga mkono mipangilio ya pamoja kati ya wizara husika (kama wizara za elimu, maji, afya, miundo msingi, mazingira, fedha na kilimo) kama njia muhimu ya kutatua shida iliyopo.
  8. Naunga mkono sheria za ukulima na mambo yote ambayo ni sawa kijamii, kimazingira na kifedha. Napinga suluhisho ambazo zinaruhusu matumizi ya GMO na mbolea za kisasa za viwandani.
  9. Kujitolea kwangu kwa huu mradi kunamaanisha nitaanzisha mjadala mbadala kwa maelezo ya kisasa kuhusu usalama wa chakula. Nitapinga maelezo duni ya shida hii na nitapinga madai kuwa Kenya iko salama kichakula.
  10. Nitatumia elimu yangu, ujuzi, nafasi yangu, mitandao ya kijamii na njia zingine zote niwezavyo kuchangia katika kuafikia haki ya kibinaadamu kwa chakula.

Join the Route to Food Alliance

Kwa kujiunga na “Route to Food” inamaanisha umejiunga na mpangilio wa kuafikia haki za kibinaadamu kwa chakula. Hadi sasa, wanaume na wanawake zaidi ya mia sita, wa rika tofauti na kutoka maeneo mbalimbali wamejisajili. Kama mwanachama wa muunguno umehalalisha Route to Food Pledge.

Privacy Policy